Aunty Ezekiel Awatolea Povu Wanaohoji Ukaribu Wake na Zari Pamoja na Wema

Msanii filamu za kibongo Aunty Ezekiel amemwaga povu kwa mashabiki Kwenye mitandao ya kijamii ambao wamekuwa wakimsema na kumuita Yuda kwa kitendo chake cha kuwa na ukaribu na Wema pamoja na Zari.Mashabiki Kwenye mtandao wa Instagram ambao wamegawanyika Kwenye team Wema na Team Zari wamekuwa wakimpiga majungu Aunty na kumuita Yuda msaliti baada ya kutangaza kwenda nchini South Africa kushiriki birthday ya Tiffah.

Kwenye mahojiano na gazeti la na Amani, Aunty alisema majungu hayo yameanza mitandaoni baada ya kusikia amealikwa kwenda kwenye bethidei ya mtoto wa Zari, Tiffah inayotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao lakini kamwe majungu hayo hayamsumbui.

Ifike mahali tufunge mjadala, kila siku ni Aunt kuwa karibu na Zari, Wema kama ni bethidei nitaenda tu. Hawa wote ni marafiki zangu sasa siwezi kubagua kwa kuwa eti Wema aliachana na Diamond wakati kule kwa kina Diamond pia kuna mpenzi wangu Iyobo na isitoshe Zari ni wifi yangu kwa upande mwingine

Kwa miaka mingi Zari na Wema wamekuwa kama paka na panya kwa ajili ya kugombea penzi la Diamond kwaiyo kitendo cha Aunty kusema anaenda Kwenye sherehe ya mtoto wa Zari kiliwashangaza watu wengi hasa kwa sababu Aunty rafiki yake kipenzo ni Wema.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*