Maimartha Aongelea Kumuita Jokate Mama wa Taifa.

Mtangazaji na mc maarufu nchini Maimartha amefunguka na kuongelea video iliyo-trend sana katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita ikimuonyesha akiwa katika hafla ya Zamaradi akimuita jokate mama wa taifa swala lililozua sana mtafaruku katika mitandao.

Maimarha anasema kuwa swala la yeye kumuita Jokate hivyo ni kwa sababu Jokate amekuwa mwanamke wa kuigwa na wanawake wengine kutokana na kujitoa kwake katika jamii hasa baada ya kuwa akifanya mambo mengi ya kunufaisha jamii.

Jokate ni mwanamke, oate ni mfano wa kuigwa,nadhani nilichokisema hata mh magufuli kakiona hicho kitu na kama mwanamke unapokuwa unajulikana tumia hiyo nafasi kuelimiesha wengine , hata kama unasema kiasi gani,haijalishi kwenye mahusiano yako uumekutana na changamoto gani.haijalishi umedondoka au umeanguka mara ngapi.she is a mom, ni mama na kuna ambao wameunganisha , Unaweza ukaiunganisha lakini naomba wasinitafutie shida..

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*