ZARI THE BOSS LADY AWAOMBA MASHABIKI KUCHANGIA UJENZI KLINIKI YA WANAWAKE

MPENZI wa mwanamuziki Diamond Platnumz kwenye ngoma ya Iyena, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’,  kwa mara ya kwanza hivi karibuni amewashukuru mashabiki zake wa Instagram kwa kufikisha wafuasi (followers) millioni nne katika mtandao huo.Zari ni mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa katika mitandao hasa Instagram na pia amekuwa mmoja wa wanawake walio nje ya Tanzania ambao wanapendwa sana.

Shukurani za Zari ziliambatana na picha picha yake iliyotumika katika video ya wimbo mpya wa Diamond wa Iyena,  Ujumbe aliouandika ni ufuatao

wapendwa wangu sina cha zaidi cha kuwalipa zaidi ya kusema asanteni sana,ninyi ni mandugu kwangu mmekuwa bega wa bega kwenye shida na raha sasa mnichangie $ 1 ili tujenge clinic ya wanawake dar,najua tukipata baba magufuli atatupa kiwanja tu PENDA SANA NYINYI, THANK YOU SO MUCH.”

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*