NAY WA MITEGO : IFIKE MAHALI UACHANE NA DRAMA ZA KITOTO

STORI ambayo imetrend kwa siku kadhaa sasa, ni kuhusu sakata la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na wanawake aliozaa nao, Zarina Hassan ‘Zari’ na Hamisa Mobeto.Ishu ni kwamba, baada ya Diamond kuachia ngoma yake mpya ya Iyena, kama kawaida yake, alianza kutafuta ‘attention’ katika mitandao ya kijamii na safari hii, kiki ilikuwa ikimlenga zaidi Zari ambapo ndugu zake, akiwemo mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ wameonekana kumpigia chapuo Zari kwamba ndiye anayepaswa kuwa mke halali wa Diamond na si Mobeto .Wakati wakimsifia Zari, wanamponda vibaya Hamisa Mobeto, wakijaribu kuiamini­sha jamii kwamba ni mwanamke asiyefaa kabisa kuolewa, hasa na ndugu yao, Dia­mond. Esma Platnumz, dada yake Diamond ndiye anayeonekana kuongoza masham­bulizi dhidi ya Mobeto.

Sitaki sana kuingilia mambo ya Diamond na familia yake kwa sababu upo msemo kwamba; Mambo ya Ngoswe, Muachie Ngoswe Mwenyewe.Wakati vuguvugu hili likiendelea, wapo watu wengi ambao wanashadadia, kila mmoja kulinganana kile anachokipenda. Wapo ambao wanatamani kuona Diamond akirudiana na mzazi mwenzake, Zari, lakini wapo ambao wanatamani kumuona Diamond akielewena na Hamisa ili baadaye waishi kama mume na mke.Lakini lipo kundi lingine ambalo halimku­ bali Zari wala Hamisa, bali linataka Wema Sepetu ‘Madam’ ndiye akawe mama mwenye nyumba pale Madale, yalipo maka­zi ya Diamond. Miongoni mwao, wapo wasanii wa kike na wa kiume, mastaa kwa maandagraundi lakini leo nataka kusema na Emmanuel Elibariki, wengi wanamfahamu kama Nay wa Mitego.

Kabla sijaendelea niweke wazi kwamba mimi si muumini wa hizi timu zinazotengenezwa kwenye mitandao ya kijamii, Team Diamond au Team Kiba kwa sababu ipo kasumba kwamba ukionekana unaongelea jambo lolote kuhusu wasanii hawa, basi lazima utahu­sishwa na timu zao.Kwa wafuatiliaji wa mambo, watakuwa wana­kumbuka kwamba wakati drama za Diamond na Zari zikilipuka upya siku chache zilizopita, Nay wa Mitego kupitia akaunti yake ya Instagram, aliandika ujumbe akimpongeza Diamond kwa kuachia wimbo mzuri wa Iyena lakini akaonesha kama kumpiga kijembe akidai kwamba am­emuacha mwanamke mwenye nyota (Zari) na kuhangaika na wanawake wanaoishusha nyota yake na kuingiza maneno mengine yasiyo­faa kuandikwa gazetini, mwisho akamalizia kwa kumwambia Diamond kwamba ataenda kumuombea msamaha kwa Zari ili yaishe na warudiane.

Siku chache baadaye, baada ya mmoja kati ya mameneja wa Diamond, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ akafunga safari kwenda mpaka Sauz kwa kile alichokieleza kwamba ni kutengeneza mazingira ya Diamond na Zari kurudiana, drama zikaendelea.Katika hali ambayo imewashangaza wengi, Nay ameibuka tena na kumtuhumu Babu Tale kwamba kwa nini amechelewa kwenda kumuombea msamaha Diamond na kusubiri mpaka yeye aandike Instagram ndiyo achukue hatua.Akaenda mbele zaidi kwa kujigamba kwamba Babu Tale anayafanyia kazi mawazo yake na hata ikitokea wawili hao wakaungana, itakuwa ni kwa sababu yake yeye (Nay wa Mitego).

Ukifuatilia drama za Nay wa Mitego, una­gundua kabisa kwamba kuna kitu anataka kufaidika nacho kupitia matatizo ya Diamond. Sitaki kuamini kwamba Nay na yeye ameingia kwenye mtego wa kutafuta kiki kwa mambo yasiyo na kichwa wala miguu.Unataka kutuambia kwamba sanaa im­ekuwa ngumu kiasi kwamba huwezi kutusua bila kutegemea kiki za ajabuajabu kama hivi? Kwa Wasafi yawezekana wameshazoe­leka sasa kwa kutafuta kiki kwenye kila wanachokifanya lakini hiyo haimaanishi kwamba ni sahihi kwa wasanii wengine nao kuanza kupigana vikumbo kisa kutafuta kiki.Kwa umri na uzoefu wako katika gemu, Nay hukutakiwa kushupalia mambo yasiyokuhusu, unajinadi kwamba Diamond ni ‘mwanao’ tangu kitambo, hivi hakukuwa na namna nyingine ya kumfikishia ujumbe zaidi ya kuposti Instagram?fike mahali uwaheshimu mashabiki zako na ifike mahali u-act like a man! Achana na kiki za kitoto.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*