MAMA MOBETO AGEUKA MBOGO MVUA YA MATUSI

Pale mtu mzima anapoingilia mambo ya watoto kisha akatolewa nishai, ni heri akajifunza kujipanga kuliko kuzidi kupoteza netiweki.Hicho ndicho kilichompata mama mzazi wa mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto ‘Tununu’, Shufaa Rutiginga ‘Mama Mobeto’ baada ya kuingilia mambo ya watoto mitandaoni kisha kuoga matusi na kujikuta akigeuka mbogo kwa wanahabari.

Baada ya Mobeto kuingia kwenye mgogoro mzito na familia ya baba mtoto wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alidaiwa kumwagwa na jamaa huyo kisha kuandikwa vibaya kwenye mitandao ya kijamii.Katika hali kama hiyo, kama mzazi bila kujua kitakachompata, mama Mobeto aliandika ujumbe mrefu kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwaomba watu, mashabiki na wazazi kuacha kumtukana mwanaye akiomba wamsamehe kwani yeye kama mama, anaumizwa mno na kitendo hicho.

Mara baada ya kuweka tu ujumbe huo, ulianza kusambazwa kwenye kurasa mbalimbali za mtandao huo mithili ya moto wa kifuu ambapo watu walianza kumshushia matusi ya nguoni ambayo hayaandikiki gazetini huku wakimtaka anyamaze maana yeye kama mama siyo busara kujihusisha na mitandao ya kijamii na kuingilia mambo ya watoto.Kutokana na watu kumshambulia kwa matusi mazito, Ijumaa lilimtafuta mama Mobeto ili kujua anachukua hatua gani dhidi ya watu hao au anajisikiaje ambapo aligeuka mbogo na kusema hataki kusikia wala kuzungumza chochote.

“Kwa kweli sitaki kuzungumza tena chochote kwa sasa, yale niliyoandika Instagram yanatosha pia sitaki kuongea kabisa na waandishi wa habari,” alisema mama Mobeto kisha akakata simu na kila alipopigiwa na kuambiwa kuwa anazungumza na mwandishi wa habari alikata simu fasta.Hivi karibuni kumekuwa na vuguvugu kubwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na habari kwamba Diamond amerudiana na mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ huku akimwacha hewani Mobeto ikiwa ni siku chache tangu mwanadada huyo alipojihakikishia kuwa na jamaa huyo.Jambo hilo lilizua mjadala endelevu, ikionekana kwamba, Mobeto siyo levo ya Zari na kwamba pumzi yake ni ndogo kushindana na mwanamama huyo raia wa Uganda mwenye maskani yake nchini Afrika Kusini.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*