BREAKING : MBUNGE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI

Mbunge wa Manispaa ya Arua nchini Uganda,  Ibrahim Abiringa, mmoja wa waliokuwa mstari wa mbele kushinikiza mabadiliko ya Katiba ya Uganda ameuawa kwa kupigwa risasi jana usiku.Polisi imesema mwanasiasa huyo wa chama tawala cha National Resistence Movement (NRM) na mlinzi wake waliuawa karibu na makazi yake kaskazini mwa mji mkuu wa Kampala na watu wasiofahamika.

Rais Yoweri Museveni amesema kuwa amesikitishwa na mauaji hayo na kuagiza maofisa wa usalama kuwasaka waliomuua mbunge huyo.

Katika mtandao wake wa Twitter Museveni, alimuomboleza mbunge huyo akisema kuwa waliotekeleza kitendo hicho wana roho ngumu.Nimepokea habari kuhusu mauaji ya kinyama ya mbunge wa Manispaa ya Arua, Mheshimiwa Ibrahim Abiriga na mlinzi wake nje ya mji wa Kampala.

Nimeviagiza vitengo vya usalama kuwasaka waliotekeleza kitendo hicho na taifa litajuzwa hivi karibuni”, aliandika Museveni.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*