MAWIGI AWATOLEA POVU WANAWAKE WANAOMTAKA KIMAPENZI DIAMOND

MSANII wa filamu za Kibongo, Mary Mawigi ameibuka na kuwatolea povu wanawake wanaomshobokea kimapenzi mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na kuwataka waache kwani anawadhalilisha na kuwafanya chombo cha starehe.

Akizungumza na Amani, Mawigi alisema kuwa, wanawake ambao wako kwenye uhusiano na Diamond au wanaotamani kuwa naye wanatakiwa kujifunza kuwa mwanaume huyo amekuwa akiwachukulia kama chombo cha starehe na akichoka anachukua mwingine hivyo wasiendelee kumkubali.

Kwani Diamond ana nini cha dhahabu ambacho wanaume wengine hawana hadi wanawake wamgombee kiasi hicho?Ninawashauri wanawake wenzangu waache kugombea au kulumbana mambo ambayo hayana faida maishani mwao, wasimame, wafanye kazi wao kama wao, maisha yataenda vizuri tu,alisema Mawigi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*