KAJALA : NITAMSAIDIA WEMA LAKINI SIYO ZARI THE BOSS LADY

STAA wa Bongo Movies, Kajala Masaja ‘Kay’ amesema anaweza kumsaidia jambo rafiki yake wa kitambo Wema Sepetu lakini siyo mzazi mwenzake na Diamond, Zari kwani hamjui wala hajawahi kumsaidia kwa lolote.Kajala amesema hayo kwenye Bethidei ya Gabo Zigamba, baada ya kuhojiwa iwapo ikitokea Wema na Zari wote wana matatizo na yeye Kajala akawa na nafasi ya kumsaidia mmoja wao anemsaidia yupi.

Sijui niongee je, lakini nitamsaidia Wema, siwezi kumsaidia Zari kwa sababu sijawahi kumjua wala hajawahi kunisaidia kwa lolote,” alisema Kajala.

Siku za hivi karibuni, ukiachilia mbali Hamisa Mobeto, Wema alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuolewa na Diamond baada ya kuachana na Zari, lakini stori za chini ya kapeti zinadati tayari Diamond amesharudiana na Zari na sasa hivi wote wapo Afrika Kusini wanajiachia na familia yao ya watoto wawili.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*