BREAKING : MCHUNGAJI AUAWA NA MAMBA AKIBATIZA

Kila ninapoona stori yoyote ni kazi yangu kuhakikisha unaiapata leo June 5, 2018 nakusogezea stori kumhusu Mchungaji Docho Eshete ambaye ameuawa na mamba alipokuwa akiwabatiza waumini wake katika ziwa Abaya nchini Ethiopia.Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa mamba huyo aliibuka kwenye maji na kuanza kumshambulia mchungaji Eshete miguuni, mikononi na mgongoni.

Mchungaji huyo alifanikiwa kumbatiza muumini mmoja tu kabla mamba hajaharibu zoezi hilo.

Hata hivyo wavuvi na wakazi wa eneo hilo walijitahidi kumuokoa mchungaji huyo mdomoni mwa mwamba lakini jitihada zao hazikuzaa matunda huku mamba huyo akifanikiwa kutoroka.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*