SIMBA WATINGA NUSU FAINALI SPORT PESA SUPER CUP,MANULA AIBUKA SHUJAA

TIMU ya Simba imefanikiwa kusonga mbele hatua ya nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup, baada ya kuinyuka Kariobang Sharks ya Kenya kwa jumla ya mikwaju ya penati 3-2 baada ya dakika 90 kumalizika kwa suruhu ya bila kufungana.

Mchezo uliokuwa uanpigwa Uwanja wa Afraha, umeshuhudiwa ukimalizika ndani ya dakika 90 huku kila timu ikishindwa kuona lango la timu pinzani wakati timu zote zikishambuliana kwa zamu bila mafanikio ya kupata hata bao moja.Baada ya dakika 90 kumalizika hatua ya upigaji wa matuta ulifuatia na Simba ikaweza kupata penati mbili zilizofungwa na Erasto Nyoni, Haruna Niyonzima na Jonas Mkude.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kuwa timu ya kwanza kuingia nusu fainali baada ya Yanga na JKU zote kutolewa jana.Baada ya Simba kuvuka robo fainali leo, Tanzania itawakilishwa tena na Singida United kesho katika Uwanja huohuo wa Afraha.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*