ANGALIA JAMAA ALIYEJINYONGA KISA MKEWE KUOLEWA NA MUME MWINGINE

Mkazi mmoja wa Manispaa ya Mityana nchini Uganda aliyetambulika kwa jina la Vincent mwenye umri wa miaka 28 amejinyonga mpaka kufa baada ya mke wake Mary Nakiboneka kuolewa na mwanaume mwingine.Andrew Musoke aliyekuwa akifahamiana na Vincent amesema kuwa marehemu amekuwa akimtumia fedha mke wake ili ajenge nyumba na baada ya kumaliza tu nyumba hiyo Nakiboneka alihamia kwenye nyumba hiyo na mwanaume mwingine.

Vincent amekuwa akiishi Gema, Bulera nchini Uganda akijishughulisha na shughuli za kilimo na amekuwa akimtumia mke wake fedha kwa ajili ya kujenga nyumba kwenye kiwanja chao” amesimulia Musoke.

Musoke anaendelea kusimulia kuwa baada ya Vincent kurudi nyumbani ikiwa imepita mwaka mmoja toka aondoke, akiwa anatumaini atahamia kwenye nyumba yake pamoja na mke wake. Alipatwa na mshangazo baada ya mke wake kumuomba Vincent amuoneshe ushahidi unaothibitisha kuwa alikuwa akimtumia fedha kwa ajili ya kujenga nyumba.Kifupi Naboneka alimfukuza Vincent na kumwambia kuwa arudi alipotoka. Lakini Vincent alimkatalia na kuamua kwenda kujinyonga kwenye nyumba” alisema Musoke.

Aidha msemaji wa  wa jeshi la polisi  mkoa wa Wamala nchini Uganda Norbert Ochom amethibitisha tukio hilo kutokea.Tulienda eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka hospitali ya rufaa ya Mityana kwa uchungzi zaidi” alisema Wamala.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*