RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP AKUTANA NA KIM KARDASHIAN

Mwanadada Kim Kardashian akutana na Rais wa Marekani Donald Trump .Kwa mujibu wa taarifa kutoka mitandao mbali mbali, #KimKardashian akutana na Trump White House kuzungumzia Marekebisho ya Sheria za Magereza.

Ajenda kuu ya Safari yake White House ni kumuombea Msamaha Mwanamke mmoja, Alice Marie Johnson ambaye anatumikia kifungo cha maisha tangu mwaka 1996 (bila kipengele cha kupunguziwa adhabu) kwa kosa la kwanza la Madawa ya kulevya na kutakatisha fedha.

Mapema wiki mbili zilizopita, rapper Meek Mill alipanga pia kutua White House kwa Ajenda hiyo hiyo, lakini kwa sababu alizozitaja alihirisha mpango wake.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*