BREAKING NEWS: ZINEDINE ZIDANE AACHIA NGAZI REAL MADRID

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Real Madrid, Zinedine Zidane ‘Zizzou’ mchana wa leo ametangaza kuachia ngazi kama Kocha Mkuu wa Madrid baada yakutwaa mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA CHAMPIONS LEAGUE).Zidane (45) alijiunga na Real Madrid mwaka 2014 akianza kukinoa kikosi cha Castilla (Real Madrid B).

Zidane alichukua mikoba ya Rafael Benitez aliyeondoka kwenye Kikosi cha kwanza hapo January 2016 .Alipata mafanikio na Real Madrid kwa mara ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuiondoa Atletico Madrid kwenye Fainali ya Michuano hiyo barani Ulaya, alipatetea Kombe hilo mwaka unaofuata na kuweka historia mpaka sasa licha yakukosa taji la La Liga msimu wa 2017-2018.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*