KAJALA MASANJA AFUNGUKA KUHUSU P FUNK,MIMBA YATAJWA

MKALI wa filamu za Kibongo ambaye ni mtangazaji wa Kipindi cha Biko, Kajala Masaja ‘Kay’amefungukia madai ya kubeba ujauzito ambao unadaiwa ni wa prodyuza maarufu wa Bongo Records, Paul Matthyasse ‘P Funk’.Kajala aliifungungukia Over Ze Weekend kuwa, amekuwa akiona maneno mengi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ishu hiyo, jambo ambalo anashindwa kuelewa limetokea wapi.

“Jamani kwa nini watu wakimuona mtu amenawiri kidogo wanasema kuhusu mambo ya ujauzito? Mimi na P (Funk) mbona wanatung’an’ganiza sana? Wanashindwa kuelewa kabisa yule ni mzazi mwenzangu?” Alihoji Kajala akisisitiza kuwa hana kibendi.

Minon’gono ya Kajala kunasa ujauzito wa P Funk iliibuka baada ya ukaribu wa wawili hao wa hivi karibuni. Kajala na P Funk wana mtoto mkubwa aitwaye Paula

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*