ANGALIA MZEE WA MIAKA 92 ALIYEITOA MADARAKANI SERIKALI ILIYODUMU MIAKA 66

Kutoka nchini Malaysia, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Dr. Mahathir Mohamad ameshinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo na ushindi wake unatajwa kuwa wa kihistoria.

Dr. Mahathir ameweka historia baada ya kukiondoa madarakani chama tawala kiitwacho Barisan Nasional ambacho kimekuwa kikiongoza nchini hiyo tangu mwaka 1957.

Kiongozi huyu ambaye ana umri wa miaka 92 baada ya kuapishwa rasmi na kuingia madarakani atakuwa ndie kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi duniani.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*