JIJI LA LONDON LATAJWA KUWA BORA KWA WANAFUNZI

Kutoka Uingereza, jiji la London limetajwa kuwa ndilo jiji bora zaidi duniani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Wachambuzi wa data wa ubora wa elimu ya juu (QS Higher Education rankings) wametaja orodha ya miji bora zaidi duniani kwa wanafunzi na kufanya London ya kwanza.

Nafasi hiyo imewahi kushikwa na miji ya Montreal ya nchini Canada na Paris ya Ufaransa. Vigezo vinavyozingatiwa katika kutengeneza orodha hiyo kila mwaka ni pamoja na soko la ajira za ndani, utofauti wa utamaduni na ubora wa maisha. Hatahivyo changamoto ya London imetajwa kuwa gharama za juu za elimu na maisha

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*