BREAKING NEWZ: MBUNGE WA MBEYA MJINI SUGU NA MASONGA WAACHIWA HURU

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wameachiwa huru kutoka Gereza la Ruanda Jijini Mbeya walikokuwa wakitumikia kifungo cha miezi mitano baada ya kukutwa na hatia ya uchochezi.

Wawili hao wamepokelewa uraiani leo Mei 10, 2018 asubuhi na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho waliosafiri hadi Mbeya kwa ajili ya mapokezi hayo.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*