SAKATA LA MWARABU FIGHTER NA MZUNGU WA HARMONIZE MAPYA TENA,MWINGINE AANIKA MAMBO

KUFUATIA nyepesinyepesi zilizopenya kwenye mitandao ya kijamii siku mbili tatu zilizopita zikidai kwamba mpenzi wa msanii Harmonize, Sarah ambaye ni raia wa Italia anatoka kimapenzi na bodigadi wa Diamond Platinumz, Mwarabu Fighter, producer wa Lebo ya WCB, Laizer amevunja ukimya na kufunguka kuhusu tetesi hizo.

Akipiga stori na kipindi cha Ndani ya Box kupitia , Laizer amesema wao kama WCB bado hawajajua iwapo ni kweli Mwarabu anatoka kimapenzi na Sarah ama ni tetesi tu.


“Sisi wenyewe tunashangaa, mnavyoona mitandaoni na sisi tunaona hivyo hivyo, hatujui kama hili jambo lina ukweli wowote, binafsi nadhani ni maeneno tu ya watu!” alisema Laizer.

Akizungumzia kuhusu kazi zake za u-producer, Laizer amesema mara nyingi hutengeneza biti bila kujali msanii gani ataitumia, ikitokea Diamond, Harmonize au mwingine akiipenda biti anaichukua na kuitumia. Lakini pia alidai huwa inatokea akitengeneza biti ya wimbo na kila msanii wa WCB anaigombania, hivyo hulazimika kuwaimbisha na anaye-fiti kwenye biti hiyo ndiye anaichukua na inakuwa yake.

Aidha, alisema mfumo wa WCB haumlazimishi msanii wa lebo hiyo kutengenezea biti palepale, anaweza kwenda studio nyingine yoyote akatengeneza biti/wimbo na yeye akaja kufanya mixing pekee. Mbali na hivyo producer huyo hakusita kuwataja ma-producer wawili anaowakubali zaidi ambao ni Selebobo wa Nigeria na Marco Chali wa Bongo.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*