RAIS WA MAREKANI AJITOA KWENYE MKATABA WA NYUKILA

Rais Donald Trump ametangaza kujitoa katika mkataba wa kimataifa wa Nyuklia wa Iran. Trump ameuita mpango huo kuwa umeoza na ni kero kwa raia wa Marekani na hauwezi kuleta amani hata kama Iran ikikubaliana na kila kitu kama sehemu ya utekelezaji wa mpango huo uliosainiwa 2015 chini ya utawala wa rais Barack Obama.

Rais wa Iran amekosoa hatua ya Marekani kujitoa na kudai kuwa haiheshimu makubaliano yake. Akienda kinyume na mataifa ya Ulaya yaliyofikia makubaliano hayo,Trump amesema kuwa watarejesha vikwazo vya kiuchumi vilivyoondolewa dhidi ya Iran kupitia makubaliano hayo ya mwaka 2015.

Trump alilalamikia mkataba huo kwamba ulikuwa unaiwekea Iran vikwazo kwa muda tu na kwamba ilishindwa kusitisha mpango wake wa makombora na kwamba Iran ilipewa kiasi cha dola Bilioni 100 kwa ajili ya kutokomeza silaha na ugaidi huko mashariki mwa kati

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*