MZUNGU WA HARMONIZE AJIBU MAPIGO,AAMUA KUFUNGUKA LIVE

MUIGIZAJI maarufu wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amemtupia dongo kali demu wa Harmonize, Sarah baada ya nyepesinyepesi kupenya kwenye mitandano ya kijamii zikidai Muitaliano huyo amemtosa Harmonize na kumchukua Bodyguard wa Diamond Platinumz, Mwarabu Fighter.
Ubuyu huo wa moto uliokuwa ukitrendi Weekend iliyopita ulidai Sarah amezima kwa Mwarabu hali hadi kufikia hatua ya kumpangishia nyumba na huduma zozote alizokuwa anapata Harmonize amezihamishia kwa Mwarabu.

Sarah na Wolper wamekuwa kwenye vita ya mapenzi huku ikidaiwa chanzo ni penzi la Harmonize na hivi karibuni walitifuana kisa Konde Boy. Lakini baada ya tetesi hizo za usaliti kusambaa mitandaoni Sam Misago Tv walimsaka Wolper na kumuuliza nini maoni yake juu ya ishu hii kumuhusu Sarah na Wolper ameishia kumtupia dongo zito Sarah:

“Duh iyo ishu mbona ni exclusive kabisa sijaisikia lakini freshi tu mbona yule demu ni Mlezi wa wana labda kachoka kumlea mwana kaamua kumchukua mwana mwingine freshi tu”.
Bifu la Wolper na Sarah lilianza baada ya Sarah kuanza kuchepuka na Harmonize wakati Wolper yupo Kwenye Mahusiano na Harmonize.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*