KAULI YA STEVE NYERERE KUHUSU WANAOULIZIA MICHANGO YA MASOGANGE

Msanii wa filamu bongo ambaye pia ni mchekeshaji maarufu Steve Nyerere, amefunguka juu ya tuhuma za kutofikisha fedha za michango zilizobaki kwenye msiba wa Agness Masogange, na kusema kuwa pesa hizo haziwezi kupewa familia.

Akizungumza na EATV Steve Nyerere amesema kwamba pesa hizo ambazo zimetajwa kuwa milioni mbili zimekusudiwa kumsaidia mtoto wa marehemu Sania, atakapoanza kidato cha kwanza hapo mwakani,

Steve Nyerere ameendelea kwa kusema kwamba familia ya Agness inapaswa kushukuru kwa mchango wao walioutoa kumzika ndugu yao, na sio kuanza kuulizia masuala ya pesa, kwani pesa hizo si kwa ajili yao bali ni kwa ajili ya mtoto.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*