IDRIS SULTAN NAYE KAMA THE ROCK,WAJIPIGIA PESA YA AJABU

Mwigizaji ( Dwayne Johnson)The Rock ni moja kati ya watu wanaonufaika na mtandao wa ‘Instagram’.
Baada ya kuachia Movie yake ya RAMPAGE hivi karibuni ambayo inaendelea kufanya vizuri, unaambiwa The ROCK huwa analipwa takribani dola za Kimarekani Milioni 1 ambazo ni sawa na zaidi ya billion 2 na ushee kwa pesa zetu za madafu kila anapoposti tangazo (promo) ya movie yake mpya katika Instagram yake.

Mchongo huo umekuja kutokana na jamaa kutegemea kutoa movie mpya mwaka 2020. Kibongo bongo @idrissultan amesema yeye ni miongoni mwa waigizaji wanaotengeneza pesa kupitia instaram japo hajataka kuweka wazi huwa anaingiza mtonyo wa kiasi gani na namna gani huwa anaingiza mtonyo huo.

Tuambie wewe unahisi ni waigizaji gani wengine wa bongo wananufaika zaidi na mtandao wa instagram?

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*