HARMORAPA AIBUKIA KWA ALI KIBA,AFUNGUKA HAYA BAADA YA KIMYA KIREFU

Baada ya ukimya mrefu msanii Harmorapa ameibuka na kueleza sababu ya kilichopelekea kupotea ghafla.

Harmorapa amesema kwa kipindi kirefu alikuwa nje ya Dar es Salaam kwa kuandaa kazi zake mpya ambazo alikuwa akizifanyia nchini Afrika Kusini.

Pia Harmorapa amedai kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii walioalikwa katika harusi ya msanii Alikiba ila alishindwa kuhudhuria kutokana na safari yake hiyo. Uongo dhambi, kualikwa nilialikwa sema nilikuwa sipo Dar es Salaam, kwa hiyo ile kuwa mbali ilisababisha kutohudhuria kwenye harusi, nilikuwa bize nasafiri sana,” Harmorapa ameiambia TV E.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*