HARMONIZE AFUNGUKA BIFU LA WILL PAUL LIVE

Baada ya kuzuka kwa taarifa za Harmonize kuwa kwenye bifu na msanii kutoka nchini Kenya, Will Paul hatimae Konde boi amekanusha uvumi huo na kusema wako sawa kilichotokea ni kutoelewana kidogo.

Story za bifu la Harmonize na Will ziliibuka baada ya Harmo kuto-support ngoma ambayo ameshirikiswa na Will “Nadhani ratiba ziliingiliana kwenye utoaji wa ngoma hiyo kwani na namie nilikuwa na ratiba zangu ila sina tatizo na Will kwa sababu siwezi kutumia muda nikarekodi wimbo, nika-shoot video halafu nisi-push, nitakuwa nimefanya kazi ya bure,” alisema Harmonize.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*