ANGALIA MAMBO YANAYOWAUMIZA WANAUME KWENYE MAHUSIANO

Kuwa Tegemezi
Wakati mwingine hata kama huna kitu lakini mwanamke unashauriwa kutojionesha huna kitu. Jioneshe kwamba una kitu hata kama huna. Wanaume wa sasa hawapendi kuwa na mwanamke ambaye kila kitu anategemea kutoka kwa mwanaume.
Hata kama huna kazi lakini ni vyema basi mwanamke akajaribu kufanya biashara ndogondogo ambazo zitampunguzia mwanaume wake makali ya kuombwa fedha kila wakati. Wanaume wanapenda kuwapa wapenzi wao fedha lakini inapozidi kipimo inageuka kuwa kero.
Yani kuanzia mahitaji ya kila siku, saluni, mavazi, ada ya watoto na mengine mengi mwanamke anamtegemea mwanaume. Yeye hataki kujishughulisha hata kidogo. Anataka aletewe, kazi yake kubwa ni kulea familia nyumbani.
Mwanaume akigundua mwanamke ni tegemezi mkiwa katika hatua za mwanzoni, ni rahisi kumkimbia mwanamke na kwenda kwa mwanamke ambaye angalau atakuwa hamtegemei kwa kila kitu. Mwanamke anayejiongeza hata kwa kutoa wazo la kuanzishiwa biashara ambayo itamfanya asiwe tegemezi.
5. Kutokuwa Muelewa
Mwanaume anapenda mwanamke muelewa. Hapendi mwanamke mbishi. Anatamani kuwa na mwanamke ambaye akimueleza kitu, anajiongeza na kufanya zaidi ya pale mwanaume alipofikiria. Mwanaume anapenda mwanamke atakayeanzisha wazo la kimaendeleo na kumshirikisha mpenzi wake ili walifanye.
Wanaume wanapenda wanawake wanaowaelewa. Kama mwanamke anakuwa si wa kumuelewa mpenzi wake, kumsaidia basi mara nyingi mwanaume humkimbia.
6. Kujigamba/Maringo
Hakuna mwanaume anayependa kutawaliwa. Wanawake wenye fedha mara nyingi wanakuwa na tabia ya kutaka kuwatawala wanaume. Anataka mwanaume afanye kile ambacho yeye anataka. Fedha zinamvimbisha kichwa na kuona kwamba anaweza kuwa na mamlaka ya kumuamrisha mumewe.
Anatumia fedha zake kama fimbo ya kumchapia mpenzi wake. Ni vigumu sana wanaume kumvumilia mwanamke wa aina hiyo, mara nyingi wanajiepusha naye. Kwa kutumia fedha zake anaweza kupata mwanaume mwingine lakini pia watashindwana katika suala la kumtawala.
7. Kuwa bize sana
Wanaume wengi hawapendi mwanamke tegemezi lakini pia wanaume haohao wanachukia mwanamke akiwa bize sana na kazi zake. Mwanaume hapendi kuona mwenzi wake anakuwa bize na kazi au biashara zake .

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*